GET /api/v0.1/hansard/entries/704913/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 704913,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/704913/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ikiwa kuna bima ya mifugo, mbona mifugo katika Kilifi wanauzwa kwa bei ya chini kwa sababu ya ukame? Je, kwa nini hakuna bima ya mifugo katika Kaunti ya Kilifi? Nikimalizia, taarifa ya Mwenyekiti inasema kuwa Serikali inafanya mipango ya kusaidia. Huu si wakati wa kupanga. Taarifa hii inafaa kuongea juu ya mikakati ambayo imewekwa kukabiliana na janga hili. Ahadi kama hizi zingefaa kama hatungekuwa na janga la njaa. Hivi sasa, janga la njaa limetukumba na lazima tutafute suluhisho. Watu wamekumbwa na baa la njaa na mifugo wanaendelea kufa ilhali hakuna suluhisho mwafaka kutoka kwa Serikali. Bw. Spika wa Muda, mzigo kama huu haufai kuwachiwa serikali za kaunti pekee yake. Hivi sasa mzigo huu umewachiwa serikali ya Kaunti ya Kilifi ambayo haikutenga pesa za kukabili baa la njaa. Je, ni mipangilio gani inaweza kufanywa hivi sasa ili kukumbana na baa la njaa linalokumba taifa nzima haswa watu na mifugo katika Kaunti ya Kilifi tukikumbuka kwamba kulingana na Katiba, maisha ya binadamu yako katika mikono ya Serikali? Serikali inafaa kuwapa watu wa Kilifi msaada mwafaka."
}