GET /api/v0.1/hansard/entries/706629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 706629,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/706629/?format=api",
"text_counter": 53,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika. Ningependa kuungana na Waheshimiwa wenzangu ili nitoe risala za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa Mhe. Paul Otuoma ambaye tunafanya kazi naye katika Kamati ya Ardhi. Tulipokea habari hizo katika Kamati kwa mshangao mkubwa kwa sababu kijana wake amekua rafiki wa karibu wa Kamati yetu. Wakati tulikuwa tukitembea hapa na pale, alikuwa anakuja kutusalimia. Kwa hivyo, hili ni jambo ambalo linashtua sana. Wazazi wote wangependa watoto wao waje kwa mazishi yao. Hakuna hata mzazi mmoja ambaye angependa kumzika mtoto wake. Kwa hivyo, tunajua ni pigo kubwa lakini tunamuombea Mola, tunaiombea familia yake, and wale watu wa Funyula ili wawe na utulivu."
}