GET /api/v0.1/hansard/entries/706731/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 706731,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/706731/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1933,
        "legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
        "slug": "rashid-juma-bedzimba"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ili nipenyeze sauti yangu kwa Hoja hii muhimu. Nawasihi Wabunge wampitishe ndugu yetu Julius Ayub Githiri kwa haraka kwa sababu ni jambo ambalo linaathiri taifa hili pakubwa, hasa katika sehemu ya Kisauni ambayo naiwakilisha. Vijana wameathirika pakubwa na mambo ya dawa za kulevya na ni vyema sana tumpitishe mwenyekiti huyu haraka ili aingie na aanze kazi yake ya kuwasaidia vijana. Taifa hili kama ninavyojua liko mikononi mwa vijana ambao, kwa idadi kubwa, wanaendelea kuathirika kupitia kwa mambo ya dawa za kulevya na ulevi, hasa kama ilivyokuwa katika mikoa ya Pwani na Kati. Maeneo hayo yameathirika pakubwa. Mhe Spika, niruhusu nisema kuwa kumpitisha mwenyekiti sio kwamba tutakuwa tumemsaidia. Bunge hili linapaswa kupitisha fedha za kutosha kuhakikisha kuwa mwenyekiti anawajibika katika kufanya kazi zake. Baada ya vijana kutumia dawa za kulevya, inakuwa kama ugonjwa wa kutibiwa. Kumchagua mwenyekiti bila kumpa fedha za kutosha itakuwa kazi ya bure kwa sababu anatakikana kutengeza mahali ambako vijana wetu watatibiwa ili watoke katika maradhi yale. Pia, Mwenyekiti wa NACADA awe na uwezo wa kuwapatia vijana fedha za kuanzisha miradi midogo midogo ili baada ya kutoka katika dimbwi la dawa za kulevya na ulevi, wawe na uwezo wa kujishughulisha na mambo mengine. Kwa hivyo, ni vyema sana kwa Bunge hili kumchagua Ayub Githiri kwa haraka kwa sababu anahitajika kule chini. Lakini pia tunapomchagua, tuhakikishe kuwa tunampa fedha za kutosha. Hii ni kwa sababu taifa letu liko mikononi mwa vijana ambao wanaendelea kuathirika; wake kwa waume. Ni hatari kubwa sana kama jambo hili halitaingiliwa ndani na Serikali na kuweka fedha za kutosha ili isaidie NACADA. Likipewa fedha za kutosha, shirika hilo litakuwa na nguvu za kuwasaidia vijana watoke katika maradhi ambayo wako nayo. Kwa hayo machache, ama mengi, nasimama kuunga mkono Hoja hii. Nawaomba ndugu Wabunge wapitishe kwa haraka Hoja hii ili bwana huyu aanze kazi yake. Ahsante sana."
}