GET /api/v0.1/hansard/entries/707095/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 707095,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/707095/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mwaka mmoja tu wa 2014/2015. Bado hatujapata ripoti ya matumizi ya pesa za mwaka unaofuata wa 2015/2016. Seneti hii inahitaji pesa za kuwapa uwezo maseneta kuzuru kaunti zao ili kuthibitisha ikiwa maendeleo yaliopo yanalingana na pesa ambazo zimetumika. Hata hivyo, kwa sababu ambazo hatuelewi, Bunge la Kitaifa limekataa kata kata kutenga pesa hizo. Tunajua kwamba kupitia Kipengele cha 96 cha Katiba, Seneti hii imepewa majukumu ambayo lazima yaambatane na pesa. Wakati Bunge la Kitaifa wanafanya hivyo, Wabunge wamejitengea mamilioni ya pesa kupitia Hazina ya National Government Constituencies Development Fund. Wametoa sababu zisizotosha za kukataa kututengea pesa. Sio lazima tuwe na tabia kama yao, kama vile ilipendekezwa na mwenzetu awali. Sio lazima uwe mshenzi ili ukabiliane na mshenzi. Ni lazima uwe na utu na hekima. Labda hatua ya kwenda mahakamani inafaa. Lakini bado tuna nafasi ya kuteua kikundi kingine ili kishiriki kwenye majadiliano. Viongozi katika Seneti hii, hasa Kiongozi wa Wengi na wale ambao wako na nafasi ya kumwona Rais wa nchi, wanafaa kutumia wakati huu kumwueleza Rais kwamba iwapo Seneti itashindwa kutekeleza wajibu wake katika nchi hii, basi yeye pia atapata lawama kutoka kwa wananchi. Hii ni kwa sababu Wakenya wanajua matunda ya ugatuzi. Seneti inapigwa vita kwa sababu tuliamua kuongeza pesa zinazoenda mashinani kupitia ugatuzi. Kule Migori ilisemekana kwamba mimi kama Seneta sionekani. Siku moja nililazimika kusema kwamba mimi sikuchaguliwa kama Seneta ili niwe nikienda kuhudhuria mazishi kila mwisho wa juma. Siwezi hata kwenda kuangalia maendeleo yanayofanyika mashinani kwa sababu sijatengewa pesa za kufanya hiyo kazi. Hicho ndicho kilio cha Seneti. Wananchi wanafaa kuelewa kwamba Seneta hajapewa uwezo wa kuzuru Kaunti kila wakati; sio ulaghai wala uzembe. Tumenyimwa uwezo huo na Bunge la Kitaifa. Huo ndio ukweli ambao wananchi wanafaa kujua. Imebaki chini ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine. Wabunge na magavana wamejificha kwa ulafi, ufidhuli kwa kutumia hela za umma vibaya. Sisi hatuna uwezo hata wa kumuajiri karani mtendaji anayeweza kuangalia stakabadhi za hesabu vijijjini. Ndicho kilio kilichoko katika Bunge hili la Seneti. Nawasihi wale tutakaoteuliwa kuenda huko, waangalie sheria kwa undani sana wasije wakatumia sababu kwamba sheria haikuundwa wala kuandikwa vizuri ilhali siku zinayoyoma."
}