GET /api/v0.1/hansard/entries/708613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 708613,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/708613/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Nakushukuru, Mhe. Naibu Spika, kwa mwongozo ambao umetupatia kutokana na ujumbe wa Seneti. Ninamuunga mkono Mhe. Duale kwa mambo ambayo ameyazungumzia hapa Bungeni. Amesema kwamba Bunge hili haliwezi kupitisha suala lolote bila kufuata sheria na sera zilizoko. Naliheshimu Bunge la Seneti na nitaendelea kuliheshimu, lakini kuna sheria ambazo zinatakiwa kufuatwa. Imebainika wazi kuwa Wanakamati wetu walioliangalia suala hilo hawakuridhika na mambo ambayo yamefanyika. Ndiposa Bunge la Taifa likaonelea kwamba sheria zilizowekwa kuhusu hundi hii haziambatani na utaratibu unaohusu hazina kuu ya taifa. Sheria hizo haziambatani na mkataba uliowekwa kuhusu usimamizi wa fedha za umma. Kwa hivyo, ninamuunga mkono Mhe. Duale. Imebainika wazi kwamba ni lazima tuwachague wenzetu 15 wajiunge na wenzetu kutoka Bunge la Seneti kwenye Kamati ya Pamoja ili walishughulikie jambo hili kikamilifu. Kwa upande wetu, ninakubaliana na mwenzangu kwamba wanachama wa Kamati ambayo ilishughulikia jambo hili hapo awali wateuliwe wakajiunge na wenzetu kutoka Bunge la Seneti ili waweze kukishughulikia kikohozi hiki. Mimi niko tayari kutoa majina kutoka upande wetu wa Upinzani ili suala hili liweze kufika katika Bunge siku ya Jumanne ili tuweze kulishughulikia haraka iwezekanavyo ndio wenzetu kutoka Bunge la Seneti wasione tunawakanyangia. Ninawaomba Wabunge wenzangu waje tulishughulikie jambo hili. Asante, Mhe. Naibu wa Spika."
}