GET /api/v0.1/hansard/entries/710532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 710532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/710532/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Wakati umefika Mhe. Duale aambiwe wazi wazi kwamba hatakuwa akipeleka ubabe wake kila pahali. Pia, wakati umefika Duale aambiwe wazi wazi kuwa ana uhuru wake wa kueleza na kutoa maoni kuhusu msimamo wake, lakini msimamo wake hauwezi kuwa sawa na wetu. Msimamo wake ni wake na wetu ni wetu. Kitu ambacho tumesema ni kwamba hatuna haja ya uchaguzi wa ugomvi. La! Tunataka amani. Kama kuna watu wanahitaji amani ni sisi. Tunataka uchaguzi wa amani. Haimaanishi tunataka kuchangia uchafu ama machafu nchini tukiamua hatutashiriki katika zoezi lolote. Katika kila kongamano na kila upande wa siasa, kuna majadiliano. Watu huzungumziana, wakaelezana na wakakubaliana. Mhe. Duale amesimama akisema: Mimi kama Kiranja wa Walio Wachache niwache kuchukua muelekeo kutoka kwa viogozi wangu wakubwa wa kisiasa. Ni wapi umeona mambo kama hayo? Hayajaonekana wala hayataonekana. Hata yeye mara nyingi, huchukua muelekeo kutoka kwa wakubwa wake. Hata wakati mwingine, tunapitisha sheria hapa na kusema hatuzitaki. Mhe. Duale The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}