GET /api/v0.1/hansard/entries/710541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 710541,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/710541/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadegu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Spika, ninakubali muongozo wako na ninaomba nimaliza kwa kuwaomba wenzetu tuelewane. Msichukue ujumbe wetu vibaya. Ninaomba muelewe ujumbe wetu vizuri kuwa kongamano hili ambalo ni la Bunge hatukulidharau wala hatujalidharau. Kongamano hili la Bunge ni la muhimu wala hatukusema halina umuhimu. Kitu tunasema ni kuwa wakati huu ambao kuna mambo mengi ambayo yanakumba nchi hii, kwa maoni yetu, tumeona si vizuri, upande wetu, kushiriki kikamilifu kwa wakati huu. Lakini, haimanishi mtu akitaka kwenda atafungiwa. Ndio maana Mhe. Midiwo amesema yeye ataelekea. Lakini, ninaomba tuheshimiane. Kama upande wetu umeonelea ndio hivyo, basi, uwachwe ufikirie uone kwa nini umeonelea hivyo. Kwa sababu Bunge linahitaji nieleze na ndio maana ninaeleza, upande wetu umeonelea, wakati huu, mambo mengi ambayo yanaendelea na kuna malumbano huko nje, huenda tukaenda chini tukaongeza malumbano. Itakuwa, badala ya kurekebisha yale tunatakiwa kurekebisha, huenda tukaenda tukachangia matatizo mengi maana utaenda na watu wataanza kuzungumziana yale yako moyoni mwao; yale yako katika fikra yao katika hali hii ya kisiasa. Kwa hivyo, maoni yetu yangekuwa, labda lingekuwa jambo la busara tuwe tumejadiliana mambo haya hapa kwanza ndio tukiwa tunaenda, tunaenda tukiwa tumewasiliana, tumeafikiana kuwa jamani, tunaenda kufanya hili na lile. Lakini, wasiwasi wetu ni kuwa tunaweza kwenda huko tukaenda tukaanza malumbano kwa sababu kila upande una mambo yake. Hivi sasa unaona mambo ya kisiasa yalivyo; tunazozana kisiasa kwa mambo ya ufisadi. Mara yanatoka upande ule, yanarudi upande huu. Kwa hivyo, hakukuwa na mazungumzo. Hata hapa Bungeni, hatukuwa na mazungumzo, na tukajadiliana kuwa jamani, tunaenda kufanya abcd na haya ndiyo mambo tunaenda kusema Kwa hivyo, Mhe. Spika, ninaomba unielewe."
}