GET /api/v0.1/hansard/entries/711040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 711040,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/711040/?format=api",
    "text_counter": 151,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nami nitoe mchango wangu kwa Hoja hii inayohusu Ripoti ya Kamati ya Mazingira. Ninaomba niseme kwamba ninaunga mkono Ripoti hii ya kuhalalisha Mkataba wa Paris. Ni jambo la kufadhaisha kusema kuwa mageuzi ya hali ya anga hayatuhusu watu wa Kenya. Maguezi yoyote ya hali ya anga yanatuhusu Wakenya kwa kuwa hata hivi sasa tukiangalia vile mambo yanaendelea na vile mvua inavyonyesha, tutaona kwamba hainyeshi kama hapo awali kwa sababu kuna mageuzi ya hali ya anga. Ni jambo la kufadhaisha kuona kuwa wakati mwingine hata sisi Wabunge husimama na kusema kuwa kitu ambacho tunahitaji ni uwajibikaji wa watu kupata ajira na kazi. Tulikuwa China mwezi uliopita. Ukiamka asubuhi utakuta uwingu umetanda angani. Si kwamba ni wingu la hali ya anga bali ni wingu linalotokana na moshi wa viwanda ambavyo vinaunda makaa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}