GET /api/v0.1/hansard/entries/711041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 711041,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/711041/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Inafadhaisha kwamba hata Serikali yetu wakati mwingine haihusiki kikamilifu. Kwa mfano, uwajibikaji uliokuwepo wa upanzi wa miti haupo tena. Umeachwa. Huko ninakotoka, Taita, utakuta misitu inakatwa kiholela. Watu wanaohusika wakiulizwa wanasema wanakata kidogo tu. Serikali, hata kupitia kwa maofisa wake wakuu, haitaki kushtumu ukataji miti katika sehemu nyingine. Kwa sasa, ninazungumzia juu ya Taita. Jambo la kuaibisha ni kwamba mkuu wa kitengo hicho cha misitu ni mtu wa kutoka nyumbani lakini analinda wale maofisa ambao wanahusika na ukataji miti. Ninaomba nichukue nafasi hii kulaani vitendo kama hivyo. Ipo miradi ambayo inafanywa ambayo inaenda kinyume na utunzaji wa hali ya anga. Mojawapo ni huu mradi wa reli ambayo inapita katika Mbuga la Wanyama la Tsavo. Hata kamati ambayo imepeana hii Ripoti ingekuwa tayari imeangalia madhara ambayo yanatokea hivi sasa huko Tsavo. Ndovu hawawezi kuvuka upande mmoja waende upande mwingine. Kwa hivyo, inawalazimu waende kwa mashamba ya wananchi. Wanapofika kule hamna lolote bali ni kuharibu mimea ya wananchi na kuwaua. Hili linasababishwa na mradi wa Standard GaugeRailway (SGR). Kuratibu Mkataba huu kunamanufaa. Sisemi kuwa manufaa hayo hayana madhara. Sharti tuangalie manufaa hayo pamoja na madhara yake. Hivi sasa, tunahimiza NEMA na vitengo vingine vinavyohusika na mambo ya mazingira vitilie mkazo kwamba watu wapande miti. Wakati ambao tulikuwa tunakata miti kiholela umeisha. Tuna viwanda vingi humu nchini lakini bado hatujapitisha sheria ya kuvilazimisha vipande miti. Ukiwa kwenye ndege angani, kisha upitie sehemu za Ngong utaona sehemu kadha wa kadha ambazo zimepandwa miti na zinaendelea vizuri. Ingawa hivyo kuna sehemu nyingine ambazo zimeachwa wazi kabisa. Hiyo inamaanisha miti ikipandwa itaweza kudumu na kufanya vizuri. Je, kwa nini hatuna sheria ambazo zitawashinikiza watu wapande miti? Kuna moshi mwingi ambao unatolewa na magari. Huu moshi ni mwingi zaidi kwa sababu ya msongamano wa magari. Ikifika jioni unapotoka kazini utajiuliza, “haya magari yanaenda wapi?” Utakuta yanaenda katika maeneo ambayo yako viungani mwa jiji la Nairobi. Swali ni, kwa nini watu wa Kenya wanaishi nje ya jiji? Kwa nini wasiishi ndani ya jiji na kufanya kazi ndani ya jiji ndiposa kule nje kuwe ni pahali pa wengine? Kwa hivyo, kama wewe umeamua unaishi jijini, hakutakuwa na msongamano wa magari maana huna haja ya kutoka jijini uende nje ya jiji. Haya ndiyo mambo ambayo tungependa tuyaangalie. Nchi yoyote huendelea kwa kuangalia vile nchi zingine zimeendelea. Haya mataifa makubwa makubwa ambayo hayakujichunga kutokana na haya madhara ambayo tunayapata sasa, yamepata shida kubwa. Kwa hivyo, itakuwa vibaya kwetu kukosa kutumia mbinu za kisayansi kujichunga kutokana na madhara ya uharibifu wa mazingira. Hatupaswi kufanya makosa ambayo mataifa mengine yalifanya ama yalipitia. Kwa maoni yangu litakuwa ni jambo ambalo kizazi kijacho hakitatusamehe kwa sababu tulijua hili jambo ni kosa na hali tunaendelea kulifanya. Mhe. Naibu wa Spika, ninaomba tuangalie mfano wa kiwanda cha Bamburi ambacho kinatengeneza simiti. Wakuu wa kiwanda hiki wana sera ya upanzi wa miti. Wana bustani nzuri yenye miti mingi na watu hupumzikia hapo ambapo kitambo palikuwa pamechimbwa. Katika nchi nyingine, sehemu za machimbo huwa zinarekebishwa na watu wanaohusika kushurutishwa kupanda miti. Hivi sasa ukienda katika maeneo ambayo mifugo inalishwa, kwa mfano, Maungu, utakuta wameambiwa wapande na wahifadhi miti. Utafika wakati waliopanda miti watafidiwa kwa hela fulani. Wanafidiwa kwa sababu wamechangia kuchunga mazingira. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}