GET /api/v0.1/hansard/entries/711042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 711042,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/711042/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ni jambo la kufadhaisha kuona kuwa sisi watungaji sheria wakati mwingine tunapotosha watu. Huwa tunawaambia eti turuhusu viwanda vijengwe na vifanye vinavyotaka. Ukweli ni kwamba viwanda hivyo vina madhara. Yale madhara ambayo yanaingia kutokana na moshi wa viwanda hivyo ni mengi. Watu wetu wataumia na tutatumia pesa nyingi kuwatibu hatimaye. Kwa hivyo, hamna haja kuwaacha watu waathirike ama wapatwe na shida eti kwa sababu haja yetu ni viwanda. Kuna mbinu nyingi za kuhakikisha kuwa vijana wamepata kazi ambazo ni nyingi. Viwanda vikiwa vinaiingia haimaanishi viingie kiholela. Sharti viingie kwa mpangilio. Pia ni sharti wenye viwanda hivyo waangalie mazingira. Pili, viwanda vikiwa vinaingia, haimaanishi kuwa viwanda vikiingia vinaachwa kiholela holela lakini viingie kwa mpangilio. Kuwe na hakika kwamba wameangalia na kuchunga mazingira; hawayaachi kiholela. Mara nyingi tunawacha mazingira yetu yanachafuliwa bila kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanalindwa na viwanda. Kwa hivyo, naunga mkono ili tuhakikisha kuwa Ripoti hii imehalalishwa na Serikali na pia kuhakikisha kuwa Kenya itakuwa mojawapo ya nchi ambazo zitatekeleza Mkataba huu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono."
}