GET /api/v0.1/hansard/entries/711190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 711190,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/711190/?format=api",
"text_counter": 301,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii uliyonipatia ili nitoe mchango wangu na nipate kuwaeleza wenzangu ambayo yalijiri. Natumaini tuliunda kitengo cha mpito wa Serikali za Kaunti wakazunguke kila pahali, waulize wananchi na viongozi wao ni wapi wangependa makao makuu ya kila Kaunti yawepo. Sisi viongozi wote wa Taita Taveta tulikuwa 497 tulikutana Wundanyi. Tulikuwa na miji yetu minne, Wundanyi, Mwatate, Taveta na Voi. Sote, kwa kauli moja tukakubaliana makao yetu makuu yawe Mwatate. Lakini kwa sababu hakukuwa na vifaa wakati huo, wakaanzia Wundanyi iliyokuwa makao makuu ya serikali za mitaa wakati huo ndio washuke Mwatate."
}