GET /api/v0.1/hansard/entries/711191/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 711191,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/711191/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Baadaye kulingana na hali ilivyokuwa, pakawa watu wakaanza utaratibu wa kuihamisha Mwatate waipeleke pahali pengine lakini wananchi wakakataa. Ndio maana Seneti ilipokutana pakawa na makosa ya kusema bado makao makuu ya Taita Taveta yabaki Wundanyi. Hayo yalikuwa makosa. Mimi kama Mbunge wa Wundanyi nikaona hapa kuna makosa. Wananchi na viongozi walikubaliana makao makuu yawe Mwatate na hayo ndiyo marekebisho yanafanywa ili makao makuu yawe katika mji wa Mwatate. Ni muhimu tusisitize yawe katika jiji la Mwatate maana kuna sehemu zingine kama Mugero ambazo zinatakiwa kuwa jiji. Jiji la Mwatate ndilo tulikubaliana kuwa litakuwa makao makuu ya kaunti ya Taita Taveta. Ndio maana Seneti The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}