GET /api/v0.1/hansard/entries/71121/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 71121,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/71121/?format=api",
"text_counter": 331,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda. Hata Mimi nasimama kuchangia mjadala huu ambao ni wa maana sana. Mengi yamezungumzwa na wenzangu na mimi nitaongezea yangu machache. Nchi yetu ya Kenya imejaa msukosuko mwingi kwa kuwa watu wanapora mali ya wengine. Zamani katika ukoo wangu, wanaume walikuwa wanalazimika kwenda kuiba ng’ombe kutoka kwa jamii ya Wamasai ili kuonyesha kuwa amehitimu kuwa mwanaume. Madam Spika wa Muda, baada ya elimu kuingia na watu kuerevuka kidogo, imekuwa vigumu kwa watu kurudia mambo hayo ya zamani. Lakini bado wizi unaendelea na hata watu wanaiba mahindi, ndizi, kuku na kila kitu. Wale ambao walichunguza kwa nini watu wanaiba mifugo ya wengine na wameandika ripoti. Ripoti hii imewasilishwa hapa Bungeni na wenzangu wamechangia maoni yao. Ndugu zangu, tukiwa viongozi, kitu cha maana ni kujua nchi yetu iko mashakani kwa tabia hii ya wizi na wale hawaibi benki, wanaiba mbuzi, wale hawaibi mbuzi, wanaiba ng’ombe, wale hawaibi ng’ombe, wanaiba mahidi, wale hawaibi mahindi, wanaiba mafuta hata wanakunywa na nchi yetu inakosa mafuta. Nataka wenzangu hapa waelewe kwamba mbali na kuwa kuna mtindo wa kiasili wa kabila fulani, kwa sababu tunaposikia jina la ubatizo; watu wanatoka na kuchukua ng’ombe za watu wengine. Serikali ikipata habari inawatuma maofisa wake kwenda kutuliza hali hiyo. Ni hao hao, Wabunge wenzangu, ambao wanaongoza wale watu tena na kusema watu wangu hawawezi kukamatwa, hii ni haki yao na hata kama wameiba ng’ombe, wapembelezwe ili warudishe pole pole. Kama mwizi ameiba halafu yuko katika sehemu fulani ya uwakilishi Bunge na hapa kuna ng’ombe ambazo wameibiwa kutoka kwa kabila lingine upande ule mwingine halafu kiongozi mwenyewe ndiye mtu wa kwanza kwenda kusimama na kuwazuia maofisa wa Serikali kuwachukulia hatua bila kuongea lugha ambayo inaeleweka na watu hawa--- Baadaye, watu wale ambao wameibiwa mifugo wanalipiza kizazi upande mwingine. Kisha, yule kiongozi tena anakimbia kwa maofisa wa Serikali ya utawala wa ndani na kulalamika kuwa watu wake wanauawa, ilhali yeye ndiye chanzo cha mambo hayo. Itakuwa jambo la maana kama tutaerevuka na kuunda nchi moja ya Mwafrika ambayo ina amani."
}