GET /api/v0.1/hansard/entries/71464/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 71464,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/71464/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, nimesimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imewasilishwa hapa na Kamati ya Bunge inayohusika na hesabu ya pesa za Serikali. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa kila mwaka ni lazima hesabu ya Serikali ikosolewe. Hii ni kwa sababu maofisa wa Serikali wamekataa katakata kuajibika na kufanya kazi yao kulingana na sheria za nchi hii. Waziri wa Ujenzi wa Umma amejaribu sana kutetea Wizara yake. Hata hivyo, ukweli ni kuwa maofisa wake wamezembea kazi. Ikiwa kazi inahitajika kutekelezwa, wao hawaitendi. Wakati wanapotenda kazi hiyo, kuna ulanguzi wa hali ya juu. Ni aibu kuona wao wanabana kila kitu mifukoni. Maofisa hawa wanapotoa kandarasi, mara nyingi wao huongeza bei ili wapate pesa zao. Ukweli ni kuwa ikiwa maofisa hawa wanaweza kuwa waaminifu kwa kazi yao, basi kandarasi hizo zinaweza kufanyika kwa bei nafuu. Mara nyingi, utaona ya kwamba hawazingatii vipimo ambavyo vimependekezwa na Serikali. Mhe. Dr. Nuh amesema ya kwamba katika karandarasi hizi, sisi kama Wakenya hatupati value for money . Ukitazama pesa ambazo zinatumika kutekeleza mradi fulani, utaona ya kwamba pesa nyingi za Serikali hupunjwa na maofisa wake. Katiba inahitaji kila ofisa wa Serikali ahakikishe kuwa utendaji kazi ni wa hali ya juu. Ni sikitiko kubwa kuona Idara mbili za Serikali kutoa gharama tofauti kuhusu ujenzi wa darasa moja. Kwa mfano, katika eneo langu la Wundanyi, Wizara ya Elimu na Wizara ya Ujenzi wa Umma hutofautiana sana kuhusu bei ya ujenzi wa darasa moja. Wizara ya Elimu hushikilia kuwa ujenzi wa darasa moja hugharimu Kshs750,000. Wizara ya Utendaji Kazi ama Wizara ya Ujenzi inasema kuwa darasa hilo lijengwe kwa Kshs1.2 milioni. Ukweli uko wapi? Haya ndio matatizo unayoyakuta kila wakati yanakumba nchi hii, na tukiendelea hivyo, hatutaenda popote. Hela ambazo zinapatiwa maofisa wa Serikali wakati wanaenda safari ama likizo ama kwa uwajibikaji katika kazi za umma, unakuta mara nyingi hawazirudishi na inatakikana akirudi kutoka safari, muda wa masaa 48, awe ametoa hesabu kamili ya kuonyesha kuwa “Nilipewa fedha za umma kiasi fulani, nimeenda safari na nimezitumia hivi na hivi na nimerudi na kiasi hiki; ama zimeisha.” Unakuta kuwa wengi wamezitumia fedha hizi kujenga majumba yao na hakuna lolote linalofanywa na maofisa wakuu wa Serikali."
}