GET /api/v0.1/hansard/entries/71466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 71466,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/71466/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kama unavyojua, Bi Spika wa Muda, tukiangalia Ofisi ya Waziri wa Fedha, ofisa mkuu katika ofisi hiyo anahitajika kila mwaka aje hapa Bungeni na aeleze waziwazi kuwa “Mwaka jana, Kamati ya Bunge ilinikosoa kwa mambo haya na haya na haya. Na baada ya mimi kukosolewa ama baada ya Wizara kadha wa kadha kukosolewa, tumeenda tukatenda hiki na hiki na hiki na tumekirekebisha hapa na hapa.” Hawaji kufanya hivyo; imewashinda! Na wakati umefika Bunge lichukulie hawa maofisa wa Serikali hatua kali. Ufujaji wa pesa za umma lazima usimamishwe na tukiendelea hivi, kusema kweli watu wa Kenya wanaendelea kupata shida. Ni maoni yangu kuwa hata fedha hizi za CDF zichunguzwe kwa undani. Fedha hizi zinapunjwa na wanaozipunja fedha hizi ni wanakamati na kila mwaka ripoti inatoka. Ripoti hii ikitokea, ni hatua gani inachukuliwa? Maofisa wangapi wa Serikali wamepelekwa kortini kujibu mashtaka kwa kufuja pesa za umma? Bi Spika wa Muda, singependa kuchosha wenzangu kwa maana wako na nia na hamu ya kutoa maoni yao. Kwa hivyo, naomba niweke tamati hapa nikiunga mkono Ripoti hii ya Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara. Asante, Bi Spika wa Muda."
}