GET /api/v0.1/hansard/entries/715889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 715889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/715889/?format=api",
    "text_counter": 251,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa muda huu. Naomba kwanza kukushukuru kwa umahiri wako. Pia nawapa kongole wenzangu kwa ukakamavu wao. Kama unavyojua, yasemekana ngoma ya vijana haikeshi. Kwa hii ngoma ya leo ya hili Bunge la watu wazima, tumeonyesha umahiri wetu. Tumeonyesha kuwa sisi ni watu wazimu. Mtu mzima huwa hawashi. Mtu mzima huzima. Twatarajia tuwe na wakati mwema. Nchi yetu ni nzuri sana. Hakuna nchi ambayo yaweza kututosheleza sisi sote. Kwa hivyo twaomba tuwe na matarajio mema katika siasa. Twataka tuwe na amani nchini. Kama nilivyosema hapo awali, hakuna nchi ambayo itatutosha sisi sote. Tukitoka mbio hapa, ni nchi gani ambayo itatutosha sote kama Wakenya? Kwa hivyo umahiri wa Bunge hili umeonyesha ya kwamba sisi twafikiria wananchi na tumewaweka mbele kuliko matakwa yetu. Kwa hivyo nawapa kongole watu wote na Seneti, kwa sababu leo kila mtu alikuwa macho wazi; kila mtu asema twawaona; mtie kidole na mtoke haraka lakini sivyo. Kwa hivyo nauombea umahiri wetu, Mwenyezi Mungu uzidi kuendelea; nawe pia Mungu akupe nguvu. Umeketi kwenye hicho kiti siku nzima kama sisi. Mawimbi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}