GET /api/v0.1/hansard/entries/715974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 715974,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/715974/?format=api",
"text_counter": 56,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa nafasi hii. Kitu cha kwanza in kwamba hili jambo tunalotaka kujadiliana ni nzito sana katika nchi yetu ya Kenya hivi sasa. Sisi kama Bunge la Seneti tukizingatia hilo kama jukumu letu, kuna umuhimu kwamba sote tuwe katika fahamu ya ripoti hiyo. Hivi sasa tunaambiwa kuwa tuingie katika msururu wa kujadiliana. Hivyo si vibaya lakini ripoti iko wapi? Hatuna ripoti katika mikono yetu. Ukishajadili halafu ripoti ije kivingine, kisheria utakuwa huna haki ya kumjibu mwenzako. Kwa hivyo, ombi langu ni kwamba tusijadiliane kwa sasa ikiwa ripoti haiko hapa ndani ya Bunge la Seneti. Tunakusihi utupe nafasi kidogo ili tuweze kujadiliana kisawasawa na kinagaubaga kuhusu ripoti hiyo. Bw. Spika, hii ni kama kunoa kisu. Ukishanoa kisu na ng’ombe na kamba viko hapo kisha umpeleke ng’ombe huyo kichinjioni, hatakubali kwa sababu kamba uliyo nayo haitafaulu hata kidogo. Huu ni mtego na sisi hatuwezi kukubaliana nao hata kidogo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}