GET /api/v0.1/hansard/entries/717372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 717372,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/717372/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Abdi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono jambo hili muhimu lililoletwa mbele ya Bunge hili la kumteuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, Askofu Mstaafu Eliud Wabukala. Wengi wameteuliwa kwa kazi hii na wakashindwa lakini leo tusijisumbue sana kwa kuzungumzia yaliyopita; tuyagange yajayo na tuangalie fursa tuliyo nayo kwamba tumebahatika kumpata Askofu Mkuu ambaye ana mafunzo na ujuzi mwingi na pia ana maadili mema. Tunajua kwamba pengine hii ndio fursa ya mwisho tuliyo nayo ya kupambana na tatizo hili la ufisadi ambalo ni saratani ambayo virusi vyake vinaenea sana katika mwili wa taifa hili letu la Kenya. Ni ugonjwa ambao, kama hatutapambana nao na kuushinda, utaangamiza taifa letu la Kenya. Najua kwamba kazi hii ambayo tunataka kumpa Askofu Mstaafu si kazi rahisi au kazi ambayo unaweza kumpa mtu yeyote. Kwa hivyo ni wadhifa mkubwa na kazi kubwa. Natarajia kwamba yeye atapata msaada anaohitaji kupambana na jambo hilo na kuweza kuiendesha kazi yake ili tuweze kufaulu katika kupambana na ufisadi. Tusipoweza kupambana na ufisadi, tutakuwa na shida kubwa katika nchi hii. Tunapoangaza macho kuangalia yaliyopita, tusiwacheke wale walioshindwa kwa sababu kushindwa kwao ni kushindwa kwetu pia. Tunamtakia kila la heri Askofu huyu mstaafu. Natarajia kwamba atafanikiwa. Akifanikiwa tutafanikiwa na nchi yetu itafaulu. Sifikiri kwamba tumepata fursa ya kumpata mtu ambaye amejaribiwa katika maisha ya kidini kama yeye alivyojaribiwa. Kwa hivyo, naomba kwamba tumteue na mimi binafsi nataka kumtakia kila la heri na baraka katika kazi yake hiyo na natarajia kwamba tutaona ataweza kutupa uongozi unaohitajika, mwelekeo unaohitajika na kuigeuza hiyo Tume iweze kutimiza uajibu wake wa kitaifa na wakikatiba katika nchi yetu. Kwa hayo machache, naunga mkono kuteuliwa kwa Askofu Mstaafu Eliud Wabukala kama Mwenyekiti mpya wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi."
}