GET /api/v0.1/hansard/entries/717607/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 717607,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/717607/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Tunakubaliana kwamba Bunge limejaribu kufanya lile ambalo lingeweza kufanya. Nina imani kuwa katika zile kazi ambazo zimebaki, Wabunge watajitolea kikamilifu kuhakikisha kuwa wameifuata ratiba yao, ambayo tutaizungumzia leo jioni ili waweze kukamilisha. Kama ilivyosemwa na mwenzangu, uongozi wa Bunge umeonelea kuwa haina haja kubadilisha viongozi ambao wanahudumu katika Kamati hii inayoshughulikia masuala ya Bunge. Tumeiacha vile vile ili iweze kuwajibika na kumaliza muhula huu ili tuendelee na kazi ambazo tumepatiwa za Bunge. Ninaomba nichukue wakati huu kuwaomba Wabunge wenzangu kuwa tujibidishe tuwezavyo ili tujumuike na wenzetu wakati huu wa kujiandikisha ili wakati wa kupiga kura utakapofika mwezi wa Agosti, kila mtu awe amejiandaa vilivyo ili kuhakikisha kuwa amerudi. Lakini ningependa pia kutoa tahadhari. Kulingana na takwimu tulizonazo, asilimia 80 ya Wabunge huwa kawaida hawarudi. Kwa hivyo, hapa huenda ikawa kuna wengine ambao watakuwa wanakunja jamvi lao na kuondoka Bungeni baada ya muda wao kuisha. Kwa hivyo, ni muhimu Wabunge wajiandae kwa vyovyote vitakavyotokea. Wengine wetu kama mimi tushaamua kuwa hatutaki kurudi kwa maana nitaomba kiti cha ugavana. Kwa hivyo, ninaagana na wenzangu polepole. Ninawatakia kila la heri katika kazi hii ambayo mtakuwa mnaifanya ili tuweze kujumuisha nchi yetu vile ilivyo."
}