GET /api/v0.1/hansard/entries/717608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 717608,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/717608/?format=api",
"text_counter": 29,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe Spika, ninaweka tamati kwa kusema kuwa kulingana na takwimu tulizo nazo Bungeni, asilimia 80 ya Wabunge huwa kawaida hawarudi. Kwa hivyo wengine watakuwa wanakunja jamvi lao wakiwa wanaondoka na kuaga Bunge. Mimi ni mmoja wa Wabunge ambao watakuwa wanakunja jamvi lao kama Mbunge wa Wundanyi maana nitakuwa ninaomba kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta. Kwa hivyo, wenzangu ninawaaga polepole wakati huu ambao nimewatumikia. Kwa muhtasari, ninawatakia Wabunge kila la heri katika kazi yao. Kwa heshima na taadhima kumbwa, ninawaomba Wabunge waunge mkono majina haya ili tuendelee na kazi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}