GET /api/v0.1/hansard/entries/718092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 718092,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718092/?format=api",
    "text_counter": 36,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika. Ninaomba nichukue nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii na mwongozo ambao umewekwa bayana ili tupate kuelekezana vile tutakavyoweza kuwa na majadiliano hapa Bungeni. Wakati huu wa kupeana mwongozo wa majadiliano Bungeni, itakuwa vyema kama kila Mhe. atakayesimama kutoa maoni yake apewe muda tukianza na viongozi wa utawala Bungeni. Tutaangalia vile waheshimiwa watatoa maoni yao ili kila mmoja apatiwe nafasi ya kutoa maoni yake katika kila Mswada ambao utaletwa Bungeni. Mhe. Spika, ni jambo la kawaida kuwa mwongozo huu ukubalike na kila Mbunge ama Wabunge wengi ili tutoe utaratibu ambao utakubalika kwa kila mmoja wetu na kwa kila kiongozi wakati wanajitayarisha. Vile nilivyosema jana, utakuwa ni muda mzuri Wabunge wautumie ili wasije wakawa katika ile theruthi themanini ya kupelekwa nyumbani na wananchi. Usipotumia muda huu utakuwa umejipotezea, na huenda ukawa na jambo muhimu la kuchangia katika Miswada hii. Kwa hayo machache, ninaomba kuunga mkono pendekezo hili. Asante, Mhe. Spika."
}