GET /api/v0.1/hansard/entries/718553/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 718553,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718553/?format=api",
"text_counter": 241,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ndiposa nimechukua Kipengele cha Saba na Kanuni 77 ya Bunge la Kenya kwamba Kiswahili ni lugha rasmi na ni lugha ya taifa na mimi ninajivunia. Kwa wale wanaodhani ni ujinga, samahani. Mhe. Naibu Spika wa Muda, chimbuko la ubinafsishaji limetoka wapi? Miaka ya 90 taifa la Kenya lilikuwa maskini. Tulikuwa waombaji. Rais alikuwa anachukua kikapu kwenda kuomba Benki ya Dunia. Waziri wa Fedha alikuwa anaenda na bakuli kwenda kuomba Benki ya Dunia. Wale wenye senti hiyo wakatoa masharti yaitwayo kwa lugha ya Kimombo, structural adjustments programmes. Hilo ndilo chimbuko la ubinafsishaji. Kumetokea tukio. Mzungu kaja na mkoba na akatushawishi tuuze reli ya Kenya. Alisema ataleta kampuni kubwa zaidi itakayoshughulikia reli ya Kenya. Tukampa fursa. Akachukua rasilimali yote. Siku ya pili, jina alilotuletea alilichukua hapa River Road. Inaitwa Rift Valley Railways. Hizi ndio athari na madhara ya ubinafsishaji wa mali ya umma. Kipengele cha 23 cha Mswada huo kimetoa wajibu kwa Bunge la Taifa kupitisha na kuidhinisha ubinafsishaji wakati unapofanyika kwa mashirika ya serikali. Kifungu cha 5 (1)(d) kinaondoa wajibu wa Bunge na kwenda kwa Baraza la Mawaziri. Hii ni dhuluma kwa Wakenya. Hii ni sheria mbaya. Utakaponiita mjinga au mwerevu, hapa nilipo, watu wa Bura walionichagua wanajua kwa nini wamenichagua na mimi naweza kujua sheria mbaya na nzuri kwa lugha yoyote ile utaleta. Nimeomba hapa mara nyingi kwamba Mswada unaoletwa hapa utafsiriwe kwa Kiswahili ili mwananchi pale mashinani wakati tunapochangia ajue sheria hii ni mbaya. Leo ninataka kuwaambia Wakenya kwamba Mswada huu ni mbaya. Ukiletwa na chama changu ni mbaya. Ukiletwa na mtu binafsi ni mbaya na ukiletwa na Upinzani Mswada huu ni mbaya na dawa ya Mswada mbaya ni kuuangusha. Mtoto wangu ataniuliza: “Kwa nini umepitisha sheria kama hii?” Nitakuwa sina jawabu la kujibu mtoto wangu atakaponiuliza swali kama hilo. Ili nilinde haki ya Wakenya na tukio lililotokea Kenya Railways, Posta na Telkom lisitokee tena katika taifa la Kenya, ninapinga Mswada huu. Wengi wanadhana kwamba ni makosa kwa serikali kufanya biashara. Ikiwa dhana ya kuleta ubinafsishaji ni kutoa Serikali katika biashara, mbona Serikali imeshika benki zote hizi. Zaidi ya asilimia 50 ya riba katika National Bank of Kenya na Kenya Commercial Bank ni ya nani? Hospitali Kuu ya Kenyatta ni ya nani? Mbona mwenyekiti kwa mkono mmoja anasema ni vibaya kwa Serikali kufanya biashara na mkono wa pili anaunga mkono Serikali ifanye biashara? Katika mataifa mengi, serikali inafanya biashara na inapata faida. Inaboresha ushuru wake. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}