GET /api/v0.1/hansard/entries/718579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 718579,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718579/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Naibu Spika Wa Muda, nashukuru kwa kunipa hii nafasi. Ningependa kuungana na wenzangu kusema napinga Mswada huu kabisa kwa sababu Wabunge wenzangu wanahitaji kuelewa tumechaguliwa na wananchi, kuwasimamia na kuangalia shida zao na masilahi yao. Hatuwezi kuenda kinyume ya wale waliotuchagua, kusema mambo yawe yakifanywa na kutoa nguvu zetu katika Bunge na kupeleka nje ya Bunge. Tutakua tukipigana na wananchi waliotuchagua. Lazima tuwe na msimamo kamili kama Wabunge kuweza kujua yale mambo tunayopitisha hapa ama yale tunaangalia. Tunaangalia mambo ambayo yanapelekana na matakwa ya wananchi na kufikiria tunafanya mambo ambayo yanafaa. Ningependa kuwajulisha kuwa, tunaendelea kutoa nguvu kwetu tukipeleka kwa watu wengine. Sisi sote tulipitisha mambo ya vyama. Hata miezi sita haijaisha watu wameanza kulia. Tumepeleka nguvu kwa wachache tumesikia wameanza kusema fulani ndio atasimama hapa and fulani ndio anasimama kule. Kwa nini tusisome yale tunayoyaona sisi wenyewe? Mambo haya tuangalie. Ninauliza, vile huwa watu wanasema katika Bunge, mmeona hata wakiwa wengi Bungeni wanatumia fikira zao kupinga mambo ambayo wanaona hayafai. Mjifunze kutoka kwa mambo hayo. Tuko kwa wale wengi na tunasema huu Mswada si mzuri. Sisi sote tuko hapa tukiwa wakilishi wa wananchi kutoka sehemu zote za Kenya. Kwa hivyo, ni muhimu tukiona mambo nyeti, tunaangalia kwa makini ili tusije kupitisha mambo ambayo tukikutana na wananchi itakua ni shida kwa sababu walitupa nafasi ya kuwawakilisha. Sisi ndio macho ya wananchi, walituchagua kwa kura nyingi na ni vizuri tubebe msalaba wetu na tukifanya makosa tutaadhibiwa kwa sababu ya kazi tulioifanya. Ndugu yangu ameongea juu ya Kenya Railways. Jambo la muhimu ambalo limesaidia nchi hii sana kwa miaka mingi ni sheria zilizokua wakati huo. Tulizivunja tukafanya tulivyofanya, ikaenda kwa wengine wachache, leo tunatafuta tutakavyofanya kuhusu Kenya Railways. Ni vizuri tusome kwa yale tunayoona yanaharibu nchi hii. Tusichukue mambo haya kama ni ya Upinzani ama ni ya upande ya Jubilee. Ni muhimu tujue tunawajibika wakati tunazungumza mambo ambayo itasaidia wananchi wetu. Napinga Mswada huu kabisa. Tumepitisha mambo mengi na yakaenda kwa wachache ambao wana mpango ya kujitajirisha wao wenyewe na kupora mali ya wananchi."
}