GET /api/v0.1/hansard/entries/718967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 718967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718967/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "vitambulisho na wale ambao hawana, wametapakaa kila mahali kwa sababu ya kupeleka ng’ombe malishoni. Ombi langu ni kuwa muda huu uliotengewa hii shughuli ya uandikishaji kura ni mdogo. Wakenya wangeongezwa muda zaidi ili wapate vitambulisho na kadi za kura. Kuna shida nyingi katika kaunti za wafugaji. Wafugaji hawana vitambulisho ijapokuwa wametuma maombi ya kutaka kupata vitambulisho. Basi, wale wanaohusika sharti wapeane vitambulisho kwa wananchi. Hii ni kwa sababu hata watoto ambao wamemaliza Kidato cha Nne hawajapata vitambulisho ilihali wamekwisha kujisajili. Cheti cha kusubiri kitambulisho hakiwezi kutumika katika kusajili kadi ya kura. Ni muhimu hivyo vitambulisho vitoke na tuwahamasishe wananchi wajisajili kupiga kura. Upande wetu sisi wafugaji, ng’ombe wamepelekwa mbali sana kutafuta malisho. Hivyo basi, wale watu ambao wanapeana kadi za kura hawajawafikia wafugaji. Wamekosa namna ya kuwafikia. Shida nyingine ni kwamba watu wetu hawana nauli ya kwenda kutafuta hizo kadi za kura. Sidhani Tume ya Uchaguzi (IEBC) itafikisha ile idadi ambayo imekusudia kusajili kwa sababu watu hawako katika maeneo yao. Ni muhimu watu wapate vitambulisho na kadi za kura kisha sisi viongozi tujitokeze kwa kuiga mfano wa Rais wetu jinsi anavyowahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kupata vitambulisho na kadi za kura. Watu wanaosajili wanastahili kupewa nauli kwa sababu mahali pengine hapana magari. Kwa mfano, watoto wetu wanalazimika kutembea kilomita 30 kwenda kusajiliwa. Kwa hivyo tushughulikie hili suala kabisa. Asante."
}