GET /api/v0.1/hansard/entries/718993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 718993,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718993/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Kura kuweza kupigwa ni lazima kuwe na vitambulisho. Na inahuzunisha kwamba mara nyingi katika Jamhuri yetu ya Kenya, utoaji na usajili wa vitambulisho umekuwa duni sana. Ni juzi tu Mhe. Rais aliona atafute mbinu ambayo inaweza kufanya jambo hili lifanyike kwa haraka. Ni vyema lakini ilikuwa imechelewa. Kwa hivyo, ningependa kutoa mwito kwamba suala la uandikishaji wa vitambulisho liwe linafanywa kila wakati na suala linafanywa bila kuwa na gharama yoyote. Watu wetu wengi hawajachukua vitambulisho hivi kwa sababu mahali vinachukuliwa ni mbali na ni gharama kupata stakabadhi hizi."
}