GET /api/v0.1/hansard/entries/718995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 718995,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718995/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Siasa ama upigaji kura ni ushawishi. Kwa hivyo, ikiwa Hoja itazungumza kuhusu kuwashawishi watu wachukue kura, tunaelekea sawa. Kwa sababu hiyo, ni lazima tukubali kwamba jukumu la kushawishi watu wachukue kura ni letu kama wanasiasa hasa Wabunge na ni jukumu la vyama vya kisiasa. Ndio maana mimi nikiwa naongoza chama changu cha KADU- Asili, nimekuwa mstari wa mbele kuzungumza na watu kwamba ni muhimu kuchukua kura. Nataka nichukue fursa hii hapa katika Bunge hili la kitaifa niseme kuwa kuna umuhimu watu wachukue kura hususan watu wetu kutoka Mkoa wa Pwani na Kaunti yetu ya Kilifi ndio wafanye uamuzi wa busara."
}