GET /api/v0.1/hansard/entries/718996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 718996,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718996/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Kumekuwa na changamoto nyingi sana katika masuala haya ya kuchukua kura. Kaunti yetu ya Kilifi, kwa mfano, imegonga vichwa vya habari kwa suala la baa la njaa. Suala hili la ukosefu wa lishe limechangia kwa kiasi kikubwa watu kutochukua kura katika Kaunti yetu ya Kilifi. Nataka nizungumze tu bila wasiwasi kuwa Serikali iko na jukumu la kuja na mbinu ya kuhakikisha kwamba watu wanaweza kupata lishe. Wakipata lishe, wataweza kuhusika katika hali kubwa ya kuweza kuchukua kura hizi. Haimaanishi watakapopewa lishe ndio lazima watapigia kura mrengo fulani. Hayo yatakuwa masuala ya baadaye. Kwa hivyo, saa hii ni kuhakikisha kwamba mbinu zimebuniwa watu wachukue kura."
}