GET /api/v0.1/hansard/entries/718999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 718999,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/718999/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Baadhi ya mikakati imewekwa kuhakikisha kwamba kura zinachukuliwa. Tumekuwa tukisisitiza kwamba ni lazima kura ziandikishwe kila mahali. Tumeona vijana wetu wa boda boda wametia juhudi na nimeona pia baadhi ya watu wanaosajili kura wamejitoa kutoka yale mashule waliokuwa wamekita kambi kuhakikisha ya kwamba wanasajili. Safari hii tunawapata wakiwa katika mahali pa kufanya biashara. Bila wasiwasi, Jumapili iliopita mimi pamoja na Mhe. Njomo tulipata fursa ya kwenda katika mazishi ya mamake Mhe. Harry Kombe. Mhe. Njomo atakubaliana nami kuwa katika mazishi haya kulikuwa na sehemu ya kusajili watu kura na watu, baada ya kuangalia mwili, walikuwa wanaenda kukamata kura jinsi wanavyotaka kujishughulisha katika upigaji kura."
}