GET /api/v0.1/hansard/entries/719000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 719000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719000/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Mtu yeyote ambaye atazungumza kuhusu kutolazimisha watu kuchukua kura itakuwa makosa. Sisi kama wakaazi wa Pwani, mara nyingi masuala kama haya hayajaenda sawa kwa sababu watu wamesema eti kura zetu ni chache. Ninataka niwahakikishie kuwa safari hii mambo yamegeuka. Watu wataendelea kujiandikisha kura kwa sababu pia nasi tunataka kuongeza uzito wetu katika masuala ya kisiasa ya kitaifa. Kwa hivyo, Hoja hii ni muhimu. Kamati ambayo inahusika katika masuala ya kisheria iko na wajibu wa kukaa chini na kuibua mbinu ambazo zitatusaidia kwa muda huu mfupi na nyingine kesho, kesho kutwa na kuendelea. Suala la kura sio suala tu la leo. Baada ya uchaguzi, labda kutokana na malalamishi ama mambo mengine, kuna uwezekano wa kuwa na uchaguzi mdogo. Ikiwa usajili wa kura utakuwa unafanywa mara moja, hivyo haitakuwa vyema. Kwa hivyo, ninataka niungane mkono na waheshimiwa wengine ambao wamesema kwamba usajili ufanywe kila wakati. Vitambulisho vitolewe kila siku na usajili wa kura uendelee kila siku. Cha msingi tunahitaji kuwaeleza watu wetu umuhimu wa kupiga kura. Mambo yalivyo sasa hivi, watu wanazungumzia zaidi kuhusu idadi ya watu wanaosajiliwa. Labada demokrasia yetu pahali ipo inazungumza tu kuhusu idadi ya kura lakini bila shaka kadri miaka inavyosonga, tutafika mahali na tutajua ni akina nani wanastahili kupiga kura na wasiostahili kupiga kura. Kwa lugha ya Kiingereza tunataka tufike mahali tutakuwa na quality voting. Hatutaki iwe kwamba kwa sababu lazima ipigwe kura, basi watu wapige kura. Mara nyingine watu hupiga kura na hawajui kitu gani ambacho wanatafuta. Kwa hivyo, hii ni Hoja muhimu. Ninaiunga mkono na zaidi ya yote, nihimize watu wangu waweze kukamata kura ndipo tuweze kuhusika katika uchaguzi mkuu ujao. Kwa hayo machache, asante kwa kunipa fursa hii."
}