GET /api/v0.1/hansard/entries/719152/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 719152,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719152/?format=api",
"text_counter": 56,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Naomba nimpongeze Mhe. Sara kwa kuleta malalamishi haya ya bararbara Bungeni. Ijapokua, Mhe. Sara naomba nikufahamishe kuwa suala hili la barabara linaadhiri kila Mbunge aliyeko hapa. Tukianzia na mimi, katika sehemu ya Bunge ninayowakilisha ya Wundanyi, tuko na kilomita moja ya lami. Tangu ilimwe na wafungwa wa Kiitaliano katika Vita vya Pili vya Ulimwengu, hatujawahi kupata lami mpaka siku ya leo."
}