GET /api/v0.1/hansard/entries/719341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 719341,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719341/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Ahsante sama Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja hii. Naunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa mara nyingi humu Bungeni. Hoja hii imejadiliwa katika Kamati mbali mbali za Bunge na katika mikutano tofauti tofauti kwa miaka mingi hapa nchini. Hili jambo linaudhi kwa sababu viongozi ambao wamepewa nafasi kuwasaidia wananchi hawaonyeshi wana kusudia kuwasaidia wananchi. Mbinu zote ziko. Ripoti zimeandikwa. Pesa ziko katika nchi ya Kenya. Haya yote yanatuwezesha kuwa na chakula cha kutosha na maji ya kutumika hata pakiwepo ukame lakini viongozi ambao wamepewa mamlaka wamekataa kufanya hivyo. Kuna ukame katika Kaunti ninayotoka. Inasikitisha. Inatubidi sisi Wabunge kufanya mengi zaidi. Unataka kama Mbunge kufanya zaidi lakini hauna hizo nguvu. Kuna mashirika kama Msalaba Mwekundu na mengine ambayo yanashugulikia wananchi. Vile vile vijana wamekuja na miradi mbalimbali kujaribu kusaidia wananchi wapate chakula na maji."
}