GET /api/v0.1/hansard/entries/719342/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 719342,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719342/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Lakini kwa ukweli, hiyo haiwezi kusaidia kwa sababu Serikali peke yake ndiyo iko na pesa nyingi za kusaidia. Wakati mwingine ninashangaa nikiona wananchi wanakunywa maji ambayo rangi yake ni kama ya kahawa. Kuna watu hawajaoga miezi mitatu imepita. Watoto wadogo wa miaka miwili na mitatu wanakaa njaa na hukula mara moja tu kwa siku. Wanakunywa uji peke yake bila sukari ama maziwa kuanzia saa tisa mpaka kesho yake saa tisa ndiyo wanakula tena. Hatuwezi kuamini watoto wetu wakipitia shida kama hiyo."
}