GET /api/v0.1/hansard/entries/719344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 719344,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719344/?format=api",
"text_counter": 248,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Ni jambo la kusitikisha na haya yote si kwa sababu ya wananchi kuwa wajinga ama Kenya kuwa nchi maskini sana. Kenya ni nchi tajiri yenye mali ya kutosha kuhakikisha kwamba wananchi hawafikii hali kama hii. Kitu kingine cha kuudhi ni kuwa viongozi hawa ambao wanapewa majukumu ya kuhakikisha kuna maji na chakula kwa wananchi wanatumia njaa kama kitega kura. Wanaenda kwa wananchi wakijisifu sana na kugawanya kilo moja au mbili za maharagwe na mahindi ama maji kidogo na kuwaambia wananchi wawapigie kura. Unashangaa sana kama hii ni nchi ambayo tumemweka Mwenyezi Mungu mbele. Hapa Bungeni, kabla tuanze kuzungumza tunaomba Mwenyezi Mungu. Kweli Mungu yuko ndani ya mioyo yetu ama ni jina tu ambalo tunataja? Katika mafunzo ya Kikristo na Kiislamu tunaambiwa tupende majirani wetu kama tunavyojipenda wenyewe, na zaidi kwa kiongozi ambaye ameapishwa na kuuamua kuwasaidia wananchi. Mwaka jana tulikuwa na Mswada huu na tukazungumza haya haya lakini hakuna jambo ambalo limefanywa huko nyanjani. Kwa hivyo, naomba kama Bunge tuwe tukiangalia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}