GET /api/v0.1/hansard/entries/719933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 719933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719933/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Kwanza, tunajadiliana mambo ambayo hatuna uwezo kuyahusu. Kila mara tunalaumu Serikali ilhali sisi ndio Serikali.Tukiwa hapa, tuna mikakati ya kisheria ya kumwita Waziri yeyote ili kuchunguza mambo ambayo tunataka yawe ni kuhusu fedha ama mabadiliko ambayo tunataka. Lakini ninaona tunalia tu bila kuona tuna uwezo wa kufanya hilo jambo. Nakubali kuna mambo nyeti ambayo tunayazungumzia hasa kuhusu serikali za kaunti. Kuna kaunti zimefanya vizuri sana na kuna nyingine ambazo zina shida. Hata hivyo, tuna uwezo wa sheria kuchunguza ni nani amekosa kufanya kazi yake. Ndugu zetu katika Seneti, mimi naona wana shida. Hii ni kwa sababu wakipendekeza na kupitisha kwamba pesa zipeanwe kwa kaunti, sisi hapa tunapitisha hilo. Mwenye kuangalia fedha akitoa ripoti yake kusema pesa zimefujwa sioni Seneti ikifuatilia. Kwa maoni yangu, Seneti iweze kusema “tulipendekeza hii na ikapitishwa, lakini hii pesa imetumika vibaya.” Pengine ni kwa sababu wengi wao wanataka kuchukuwa hivyo viti vya magavana. Nafikiri ndio maana hawataki kuunda sheria itakayochunga hizo pesa. Tunazungumza mambo ya kupatia makaunti pesa lakini hatujadiliani kuhusu ile pesa wanayokusanya. Hatuoni wala hatusikii. Hizo pesa ni zao za kula. Ni pesa za wizi na za kufujwa. Mbeleni kulikuwa na mabaraza ya miji na manispaa . Mfano ni manispaa ya Nakuru ambayo ilikuwa ikijisamamia bila kupewa pesa na Serikali. Wakiongezewa ilikuwa ni pesa kidogo kutoka kwenye hazina ya Local Authority Transfer Fund (LATF ). Sasa hii wanapewa pesa nyingi na Serakili lakini Maseneta hawafuatilii pesa ambazo wanatoza watu ushuru. Ni muhimu Seneti ifuatiliie kwamba Kenya Revenue Authority (KRA) iwe ikitoza ushuru."
}