GET /api/v0.1/hansard/entries/719935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 719935,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/719935/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngujuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Kwa sababu nazungumzia jambo nyeti. Itakuwa bora tukipitisha sheria kuwa pesa zote zinazokusanywa katika makaunti ziwe zikiwekwa na Serikali mahali fulani. Hizo pesa zitakuwa ni zao tu lakini tujue zile wataongezewa na zile wamekusanya ni ngapi. Bila kufanya hivyo, tutazungumza mengi na tutaendelea kuwa na shida kubwa. Kwa hivyo, ninaunga mkono huu Mswada lakini tuweke mikakati ya kutosha ili tuweze kujua pesa ambazo zinatozwa ushuru ni ngapi. Tunasikia kwamba hata zingine haziwekwi kwenye akaunti ya kaunti. Hizo pesa zinapatiwa mawakala ambao wanakusanya hizo pesa. Baadaye hizo pesa hazirudi kwa wananchi hata kidogo. Hayo ndiyo maoni yangu na ninashukuru kwa kuniongezea muda."
}