GET /api/v0.1/hansard/entries/720022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 720022,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/720022/?format=api",
    "text_counter": 53,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Pukose",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": "Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao ni wa kuzuia watu kuteswa kwa njia ambazo hazifai. Tunajua kwamba miaka ya 1990, Wakenya wangeshikwa na Special Branch na kuhusishwa na mambo ya siasa. Walimu wa vyuo vikuu na wanafunzi pia walishikwa kwa tuhuma za kupindua Serikali. Waliitwa “Mwakenya”. Hayo mateso yaliendelea hata katika sehemu zingine. Ndiposa sisi kama Wakenya tunaleta sheria za kuangalia kwamba wale wanaoteswa kwa namna moja ama nyingine wanapata ridhaa. Kwa mfano, kule Endebess, kuna jamii ambayo ilidhulumiwa miaka ya sabini na themanini. Ikiwa unatoka jamii ya Sabaot, wanasema wewe ni Mganda. Unashikwa, unawekwa kwa gari na unabebwa mpaka Malaba. Wanasema wewe ni mtu wa Uganda na unakosa namna ya kurudi nyumbani. Unaenda unapitishwa kule sehemu za Mbale, unarudishwa na wewe ni mtu wa kutoka Endebess. Ndiposa, ninaposikia viongozi wengine wakisema kuna jamii ambao siyo Wakenya inapewa vitambulisho, inatukumbusha kwamba tunarudi kwa yale mateso jamii ya Sabaot ilipata miaka ya sabini. Waliitwa Waganda na kupelekwa Uganda kwa mateso. Nafikiri kiongozi kama huyo hana kichwa sawasawa. Mateso yanapoingia katika jamii, inaendelea kwa vizazi vijavyo. Ni lazima tujaribu kuheshimu uongozi na raia ya Wakenya. Huu Mswada unatupa nafasi ya kuangalia kwamba mtu anapoteswa kwa namna moja ama nyingine na apelekwe hata nchi nyingine, tunaweza kupata ridhaa. Huyo mtu anaweza kulipwa kwa njia gani wakati anaporudi hapa. Kwa hivyo, mimi niko tayari hii sheria The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}