GET /api/v0.1/hansard/entries/720023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 720023,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/720023/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Pukose",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1458,
"legal_name": "Robert Pukose",
"slug": "robert-pukose"
},
"content": "itakapokuwa tayari, wale watu wetu ambao waliteswa kwa namna moja au nyingine na kupelekwa sehemu zingine, tutakusanya majina yao ili walipwe ridhaa. Tunapoongea mambo ya mateso, kuna wale ambao wameteswa sana. Pengine ilikuwa jamii inayoishi sehemu fulani na ikahamishwa kwa lazima. Sisi kule Trans Nzoia, katika miaka ya sabini, katika sehemu moja ambayo inaitwa Kaptegat, na juzi juzi katika sehemu kama Timboroa, watu walifurushwa kutoka msituni, wakateswa, manyumba yao yakachomwa na wakapigwa na askari wa Serikali ya wakati huo. Mhe. Spika, tutaiangalia kwa makini sheria hii ili tutakapoipitisha, tujue wale walioumia miaka iliyopita watafidiwa namna gani. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}