GET /api/v0.1/hansard/entries/721038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 721038,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/721038/?format=api",
"text_counter": 633,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Ninashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Pili, ningetaka kumpongeza Mhe. Okoth kwa kuuleta Mswada huu wakati ufaao. Haswa, kwa ujuzi ninao, kwa mambo nimepitia, Mswada huu unahitajika sana na ni muhimu sana sisi kama Wabunge tuuangalie kwa makini. Mara nyingi, Miswada huja hapa Bungeni na tunaikimbiza bila kuangalia matokeo yake. Njia za kuwaadhibu washukiwa kama wameshikwa na polisi zimezidi kila mahali. Polisi wanatumia njia nyingi sana. Matusi ambayo wananchi ambao tunaongoza wanatusiwa ni adhabu kubwa sana kabla hawajafikishwa kortini. Wanatusiwa vibaya sana. Polisi wanawatukana wananchi kwa majina ya waheshimiwa na watu wengine wakubwa. Ni kama hawa ndio mwisho. Ukishikwa na polisi, ni kama umefika mwisho. Ningetaka kutoa mfano wangu mwenyewe. Wakati tulishikwa, ambao tunajulikana kama Pangani 6, kuadhibiwa ambako tuliadhibiwa bila kupelekwa kortini kulikuwa ni kwa hali ya juu zaidi. Kama Mbunge ambaye anaheshimiwa na amechaguliwa na watu anawekwa seli na hawezi kupewa maji, anapewa ndoo ya kuenda choo mukiwa na wengine huko ndani, huwezi badilisha nguo--- hii ni adhabu ambayo haitakikani. Ndio ninasema Wabunge wajaribu kuangalia jambo hili sana. Nyinyi Wabunge kwanza ningeomba muanze kuelewa. Uhusiano wenu na polisi uko na shida. Wakiona Mbunge sijui ni kama uliwafanyia kazi gani. Inakuwa matusi ambayo haifai The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}