GET /api/v0.1/hansard/entries/721039/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 721039,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/721039/?format=api",
    "text_counter": 634,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "kwa mtu ambaye anaheshimika. Kama Mheshimiwa ataadhibiwa na matusi kama hayo, mwananchi wa kawaida, wale tunaongoza, hali yao itakuwa namna gani? Pia, kunyang’anya watu mali yao baada ya kushikwa na kuingizwa seli ni kuadhibu mtu kabla hajafika kortini. Unakuta hata njia ya kupea hawa watu chakula, wengi wanaadhibiwa kwa majina ambayo hata siwezi kutaja hapa kwa sababu lugha hiyo ni mbaya kwa Mbunge kutaja. Lakini unakuta wanaadhibiwa vibaya sana. Hata rumande zingine ukiingia hali ni mbaya sana. Kwa hivyo, lazima tuangaliie mikakati. Nafasi imekuja ya sisi tuangalie huu mjadala na tuangalie ni kitu gani tutaweka kisheria ili kulainisha vifungo ambavyo tunaweza ongezea. Kwanza hasa wakati huu tunaenda kwa siasa. Na ile siasa tunaenda, nawahakikishia nyinyi Wabunge, polisi wanawangoja. Matusi mtapata na kuadhibiwa na kufungiwa mikutano ovyo ovyo. Hivi vitu viko hapa. Ni kama wakati wa kuvuna mahindi. Wakati wao wanasema umefika. Licha ya hayo, kuna polisi tunaheshimu kwa sababu utaratibu wao ni mzuri. Wanaheshima, wakitaka kukuletea summon s kuna utaratibu mzuri. Lakini kuna wengi ambao njia zao lazima tuzikatae kama Wabunge na tuweke sheria kali, wataadhibiwa namna gani. Tumeona wengi wakifa katika seli; tumeona wengine wakibakwa wakiwa kwa seli; tumeona wengine wakiadhibiwa kwa njia ya matusi; na tumeona wengine wakiadhibiwa kwa kunyang’anywa mali yao. Hayo yote tumeyaona. Wakati umefika. Juzi niliona kwa NTV, ulaghai wa polisi wa trafiki. Niliona wakiokota pesa kwa wananchi na nikajiuliza kama huyu mtu amewekwa kuchunga maisha ya raia ama amewekwa hapo--- Niliona polisi mmoja ambaye kijiti chake kimewekwa Big G upande wa chini ndio noti ikiangushwa chini, inachukuliwa kwa hicho kijiti. Mambo haya ndio yako kwa seli na yana madhumuni ya kuadhibu watu wetu. Ni mambo ya aibu. Nauliza Wabunge tuweke mikakati ya kutosha kwa Mswada huu ili tusaidie mwananchi wa kawaida. Kama wewe utaadhibiwa kama Mbunge, unafikiriaje mtu yule wa chini? Wengi wanakubali mambo fulani yafikishwe kortini ili waondoke kwa seli. Sio kwa sababu wamekosa, lakini wanakubali ili waondoke kwa seli. Afadhali waende kortini ama wapelekwe rumande kwa sababu ya ile adhabu iko kwa seli. Kwa hivyo, utaratibu wa kujua mtu kama amefanya makosa sio kumwadhibu, kumpiga au kumnyang’anya mali yake. Kuna utaratibu ambao unahitaji kufuatiliwa. Jambo muhimu tungeomba Wabunge wenzangu ni tuangalie sana jambo la kutozwa faini au kifungo kwa mtu anayemuumiza Mkenya bila sababu. Kuchukua sheria mikononi mwako--- Sehemu zingine unawekwa stesheni ya polisi kabla ya kupelekwa kortini na utahukumiwa huko, utapigwa faini huko, utaachiliwa huko ama utaadhibiwa huko huko ndani. Kwa hivyo, ninaunga mkono jambo hili ili tuweke mikakati. Mhe. Okoth, Mungu akubariki sana."
}