GET /api/v0.1/hansard/entries/721273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 721273,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/721273/?format=api",
"text_counter": 231,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Nashukuru Mheshimiwa Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia nami nitoe mchango wangu kuhusu hawa ndugu na dada zetu ambao wamependekezwa ili wapewe kibali na Rais tukianzia na Bunge ili nao waingie kazini na kuwapa Wakenya matumaini ya kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki maana hivi sasa hatuna Tume nzuri. Tunataka kina Hassan waondoke na ni muhimu sisi kama Bunge tumalize zoezi hili ili tuwape Wakenya kwa ujumla nafasi ya kupiga kura ifikapo August. Nikiangalia orodha ile ambayo tumepatiwa hapa Bungeni kuanzia Mwenyekiti na wenzake, naona kuna usawa ambao umependekezwa kati ya wanawake na wanaume ili tufuate vile Katiba inavyosema. Mambo ya maadili hayajatolewa wazi wazi. Hamna mtu ambaye ameenda kwa Kamati ambayo ilikuwa inawahoji kuzungumzia kwa undani kuhusu swala la maadili na nidhamu. Kuna mmoja wao ambaye alikuwa ana wasiwasi kuwa maadili ya hawa ambao wamependekezwa kuwa huenda ikawa ni tisho au huenda ikawa inaleta cheche zozote. Bali, tukisoma ripoti ya Kamati inaonyesha kuwa wote ambao wamependekezwa walikuwa wamehitimu, kitu cha kwanza, maadili yao yaliridhisha, ya tatu wana uzoefu ijapokuwa pia mna swala ambalo limeandikwa mara kwa mara kuwa labda hawana uzoefu. Lakini inategemea ni uzoefu wa aina gani. Tukiangalia hawa wote tukianzia na Mwenyekiti, ni watu wamehitimu wamesoma, ni watu ambao wamefanya kazi, ni watu mara nyingi wamepewa shughuli kadha wa kadha na wakazifanya, wakazitekeleza na wakazitimiza bila shida yoyote. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}