GET /api/v0.1/hansard/entries/721274/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 721274,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/721274/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Katika hao wote ambao wamependekezwa, naomba niwe wazi kuwa wawili wao ni watu ninawafahamu sana. Nitaanza na Wanjala. Yeye ni binti anayetoka Taita ijapokuwa ni mzaliwa wa Kwale. Babake ametoka Sungululu katika Wilaya yangu pale ambapo mimi mwenyewe nawakilisha kule Wundanyi, akahamia Kwale na bintiye akazaliwa lakini amerudi huko Taita. Ni binti ambaye namfahamu na ana uadilifu wa kutosha kwa hivyo hapo sina wasiwasi. Nina imani kuwa atatekeleza wajibu wake na atafanya kazi na imani sawa. Nikiangalia huyu mwingine ambaye watu wanaanza kushangaa ni nani ni dada yetu Consolata Nkatha Bucha Maina. Nimemfahamu akiwa mwanafunzi miaka themanini nikiwa wakati huo ni Meneja katika Industrial Development Bank. Nimemfahamu akiwa mtoto mwanafunzi akiomba kazi. Amefanya kazi wakati huo wote hata wakati ameenda Kenya Wildlife Service (KWS), nilikuwa consultant kule na ninafahamu kuwa ana uadilifu. Mara nyingi watu wanaweza kuuliza unawafahamu aje hawa watu? Ninawafahamu kwa sababu ya uzoefu wangu wa kazi. Nikiangalia kama Duale hana uzoefu kama ule nilionao ndio maana wakati mwingine anaanza kutia wasiwasi lakini ule uzoefu nilio nao na umri nilionao nimeona mengi, nimekutana na wengi na nimeangazia mengi. Kwa hivyo, sina wasiwasi wakati huu kwa kazi ambayo imefanywa na Kamati yetu ya Sheria. Ni kazi ya kuridhisha na watu ambao tumewapatia. Tukiangalia ule muda tulionao hata tukianza kusema kuwa tutafute wengine, huo muda tulionao wa kufanya uchaguzi August ni muhimu tumalize hili zoezi ili waingie kazini. Lazima Wakenya tuweze kuwa na imani na Wakenya wenzetu. Kama kila wakati hatutakuwa na imani na Wakenya wenzetu, itakuwa inatuletea shida. Labda ni kama haya ambayo yalikuwa yanasemwa hapa wakati tulikuwa tunatoa maamuzi kuhusu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Ufisadi. Watu wengi walikuwa na wasiwasi. Wasiwasi wangu ni kuwa je tunamjaribu mtu wa Mungu katika kazi ambayo itamletea vishawishi na baadaye tuingize Kanisa katika shida? Huo ndio wasiwasi nilikuwa nao. Mpaka sasa ninao. Lakini kwa hawa ambao wanaenda kuangalia mambo ya usajili wa kura, kusimamia uchaguzi na kuhakikisha kuwa nchi hii inafanya uchaguzi wa haki ambao utakubaliwa na kila mtu, sina wasiwasi kuwa watatekeleza wajibu wao na wataweza kufikisha nchi mahali iliko. Naomba nichukue nafasi hii pia kuwahimiza Wakenya. Bunge linatimiza wajibu wake. Wakenya nao watimize wajibu wao wa kujitoa waende wajiandikishe, wajisajili kuwa wapigaji kura maana haina haja tupitishe hawa, sisi kama Bunge tuna imani watafanya kazi, na hawatashindwa kujiandikisha wawe ni watu wachache halafu uchaguzi utakuwa umefanywa na idadi ndogo sana ya Wakenya ikilinganishwa na ile inatakikana. Tunaomba Wakenya, wakati huu ambao umetolewa na IEBC, wachukue wakati huu waende wajiandikishe. Nasi kama Bunge, tunakamilisha zoezi hili leo. Nina imani Wabunge wenzangu tutaunga mkono mapendekezo ambayo yameletwa hapa na Kamati hii ya Sheria ili tukamilishe na Rais awapatie kibali waanze kazi hata ikiwezekana kesho kutwa na hao wengine wafunge virago waende. Kwa hayo mengi naomba niunge mkono wote ambao wamependekezwa katika Ripoti hiyo."
}