GET /api/v0.1/hansard/entries/721330/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 721330,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/721330/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Asante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi niweze kuchangia na kuunga mkono uteuzi wa makamishina wa Tume ya Uchanguzi. Ningependa kumpongeza Mhe. Rais kwa uteuzi wake wa makamishna hawa. Ni dhahiri kwamba tunapoenda kwa uchaguzi mwezi wa nane matokeo yataweza kukubalika kwa pande zote za vyama ikizingatiwa kwamba wengi wa makamishina walikuwa kwa mrengo ule mwingine. Hivyo basi, ninataka kusema kwamba tunaunga mkono Hoja hii, si kwa sababu kamishna fulani anatoka eneo bunge lako. Tunafanya hili kwa sababu ni Mkenya anayestahili, na ako na stakabadhi zinazotosha kwa kazi hii ambayo ameuliza kupatiwa nafasi kuweza kuhudumu. Tunafanya haya ili tuwe na uchaguzi ambao ni wa kuaminika, na matokeo yake yatakubalika na watu wote. Kile ambacho kimefanyika sasa ni kwamba wenzetu ama upande ule mwingine umepewa hiyo nafasi ya kuandaa uchaguzi. Ni matumaini yetu kwamba viongozi wa upande ule mwingine watakubali hayo matokeo. Hii ni kwa sababu uchaguzi utaanza mapema asubuhi na saa kumi na mbili na nusu jioni, utakuwa umeisha na mwenye kushinda atajulikana. Hatungependa kuona watu wakienda kuketi barabarani kuandamana hapa na pale na kusababisha uharibifu mwingi wa mali na hata upotezaji maisha kama ilivyokuwa mwaka wa 2007/2008. Mhe. Spika, ningependa kusema asante kwa uteuzi ambao Mhe. Rais Uhuru Kenyatta amefanya. Ninaunga mkono."
}