GET /api/v0.1/hansard/entries/721715/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 721715,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/721715/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Nataka kuunga sana mkono Mswada huu mwanzo kama mwakilishi wa vijana katika Bunge kwa sababu Mswada huu utawasaidia wale ambao ni wanyonge zaidi katika jamii kama wanawake, vijana na walemavu. Mswada huu unaruhusu wananchi kuomba mikopo kutoka kwa benki za kawaida kwa njia ambayo ni rahisi. Kawaida wananchi wakiwa wanataka senti ama mikopo, inabidi waende kwenye vyama vidogo vidogo vinavyoitwa microfinance katika lugha ya Kiingereza ambavyo wakati mwingine vinalipisha faida kubwa sana ama interest . Kitu kingine ni kuwa, kwa sababu katika Serikali, hivi sasa hatuna mambo ya elimu bure mpaka shule za upili na kadhalika na kwa sababu pia mambo ya afya yamekuwa ghali sana, unapata inawabidi wananchi waende kwa watu wa rehani kuweka mali yao ili waweze kupata mikopo. Watu wa rehani huwa wanalipisha faida nyingi sana na badala ya kumsaidia mwananchi, inamweka kwenye umaskini zaidi. Mswada huu unaruhusu watu wapate mikopo kwa benki na si lazima watumie ardhi na nyumba kama tunavyojua. Tunajua kuwa katika nchi yetu ya Kenya, kupata cheti cha ardhi au The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}