GET /api/v0.1/hansard/entries/722250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 722250,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722250/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii. Hiki ni kipindi muhimu sana cha kuzungumuzia maswala ya pesa za umma. Kama Sen. Elachi ambaye ninamjua kwa siku nyingi, ninaunga mkono Hoja hii. Kama kaunti zetu zingekuwa zinafanya kazi ningeishtumu Serikali Kuu sana. Lakini Serikali hii ina bahati kwa sababu katika kaunti nyingi swala la ufisadi ni kawaida. Magavana wengi wanaendeleza ufisadi na uporaji wa mali ya umma. Kiwango hiki cha pesa za kaunti zetu ni cha chini sana. Ikiwa kaunti zingelikuwa zikitumia pesa vizuri tungependekeza kiwango hiki kiongezwe. Hata kama tungetaka waongezewe kwa kiasi cha Kshs1 millioni au Kshs1 billioni, swali muhimu hapa ni hili: Je, wananchi wetu wamepata huduma ambayo ililingana na pesa tulizowapa magavana? La. Hakuna chochote kilichofanyika mashinani. Hakuna hata alama moja ya kuonyesha ya kwamba pesa tulizopitisha hapa zilifanyia wananchi kazi. Serikali ya Jubilee haifuatili kwa makini na kuona kwamba wanaofuja pesa za umma wanachukuliwa hatua. Inawezakanaje kuwa gavana ambaye akichaguliwa alikuwa na gari moja na sasa na magari mengi? Boma yake ilikuwa na nyumba moja na sasa ana nyumba za kifahari nyingi zenye vyumba vingi. Mambo haya yote yamefanyika kwa muda wa miaka miwili. Isitoshe, anaweka ua ya stima, anaanza kujenga majengo ya biashara na kadhalika. Hata hivyo, Serikali ya Jubilee inakodolea mambo yote haya macho bila kuchukua hatuayoyote. Ni kama kuna mahali pesa zinachimbwa na kutumiwa ovyoovyo. Mtu akishapewa nafasi ya utumishi wa umma, anajitajirisha mwenyewe. Hili hutendeka hasa mtu anapokuwa msimamizi wa fedha za umma. Huwa anajifanya ni kama amepata mgodi wa kuchimba pesa na kuzitumia kama anavyotaka. Hii si tabia za magavana peke yao. Tunaona hiyo tabia hata kwa viongozi wa juu katika Serikali ya Jubilee. Kwa mfano, haya yanafanyika na Naibu wa Rais na wengine. Majengo yameanza kujengwa katika kila pembe za nchi hii. Fedha za umma zikiwa zinatumika lakini hakuna mtu anauliza jinsi mtu ambaye mshahara wake ni Kshs100,000 anaweze kujenga nyumba za gorofa ishirini na zaidi. Haya mambo Sen. Muthama, Sen. (Prof.) Kindiki na wengine hatuwezi kufanya hivo. Wengine walikuwa hawana hata ofisi ya kibinafsi kabla ya kuchaguliwa lakini sasa wanaanza kufanya mambo ya kiufalme bila aibu. Serikali ya Jubilee bali na kuwa na vitengo vya kuchunguza na kuangalia ni nani anahujumu uchumi wa nchi kwa kuharibu mali ya umma, inakaa tu ni kama hakuna chochote kinatokea. Nchi ya Kenya inaweza kuongozwa na mtu yeyote. Inaweza kuongozwa na karani, watu wanaofanya kazi ya kufagia barabarani ama wahudumu wa hospitali. Kama kuna watu ambao ni watiifu na wanaweza kuvumilia shida, ni Wakenya. Ikiwa mtu anachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara na baada ya miaka miwili au mitatu anakuwa tajiri kuliko watu wa kaunti yote waliompa kura, basi hii ni nchi ya kiajabu. Mimi ninaiombea hii nchi na kuwaombea Wakenya. Naomba mwenyezi Mungu aitazame Kenya kwa sababu wanawe wanateswa sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}