GET /api/v0.1/hansard/entries/722252/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 722252,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722252/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sen. Elachi na Sen. Kagwe wamesema watu hawapati matibabu katika hospitali za umma. Nikizungumuzia ugawaji wa pesa inayoenda kwa kaunti kwa mara ya mwisho katika kikao ya mwisho ya Bunge hii, ilikuwa ni kosa kubwa sana kugatua mambo ya matibabu. Shida tulio nayo leo ni kwa sababu hawa magavana hawajui ya kwamba kuna Serikali ya Kuu na Serikali za Kaunti. Hawajui ya kwamba Serikali za kaunti hazina uwezo wowote. Haiwezi kufanya kitu chochote bali kuwatumikia wananchi na kutoa huduma inayohitajika. Wao wamepewa kaunti, wameweka magari zao ving’ora, wameandika askari wa kuwalinda, wamenunua zulia nyekundu na kuweka katika magari yao. Utawapata hata wakibeba vyoo vyao kama Rais wa nchi. Wanafanya kila kitu ni kama wana mataifa yao inayojulikana kama kaunti. Wanasahau ya kwamba kuna Serikali Kuu ambayo ina Rais. Magavana ni watumishi wa umma ambao wanastahili kutoa huduma peke yake na kufanya kazi kama punda. Lakini, hao wamekuwa ni watu wa kutembea kila pembe. Wake zao wanafurahi wakiitwa “Mama Kaunti” halafu wanapewa vyeo kama vya Rais. Hawa watu wamekosa. Wameshindwa na kazi yao na ninawashutumu kutoka sasa hadi dakika ya mwisho. Ugatuzi usiwekwe katika mambo ya matibabu. Kama tunataka ugatuzi katika kaunti zetu, hawa magavana waambiwe wajenge zahanati peke yake. Wanaweza kujenga dispensari. Mambo ya kuleta daktari, madawa na mitambo ya kuhudumia wagonjwa iwe ni kazi ya Serikali Kuu. Madaktari na wahudumu wa hospitali wote wapige foleni kwa Serikali Kuu ili wapewe mishahara ya juu. Kazi ya magavana iwe ni kujenga zahanati pekee. Hii ni kwa sababu wasipojenga, wananchi hawatajua kama wanafanya kazi. Ni afadhali wapewe hiyo jukumu ndio wakiiba, waibe pesa hizo za ujenzi. Lakini wasipewe jukumu ya kununua madawa na vifaa vingi vya hospitali. Mheshimiwa Uhuru Kenyatta anajificha pembeni kwa sababu mambo ya afya ni ya serikali za ugatuzi. Hawezi kuulizwa swali lolote kuhusiana na mambo ya afya. Ingelikuwa ni kazi ya Serikali Kuu, tungeenda mbele ya Mheshimiwa Rais na kumuuliza maswali mengi. Kwa mfano, je, inakuwaje madaktari wanagoma na wewe bado tunaona ukipiga muziki na kucheza na vijana kule Ikulu? Lakini kwa sababu si jukumu lake, Wakenya wanaendelea kuteseka. Majukumu haya yamepewa watu ambao hawawezi kuyatimiza. Ningependa huduma hizi zitolewe katika serikali za kaunti na ipewe Serikali Kuu na vile maswala ya elimu yalivyo. Hawa magavana walikuwa wanapiga kelele wakitaka ugatuzi wa elimu. Walitaka maswala ya walimu yawe mikononi mwao. Hawa magavana wanaobeba pesa mchana kutwa, itakuwaje wapewe jukumu la kuwalipa na kuwaangalia walimu wanaowasomesha watoto wa maskini? Hiyo haifai. Inafaa kuwa jukumu la Serikali kuu. Swala la walimu na mishahara yao ishughulikiwe na Serikali kuu. Nao magavana na serikali za kaunti wajenge shule pekee; zile za chekechea, msingi na upili. Kama sio hivo, nchi hii itaumia. Nakubaliana na Sen. Elachi vile alivyosema kuwa Rais Mstaafu Mwai Kibaki alijenga barabara katika taifa hili. Alifanya kazi inayoonekana. Lakini kazi ya Jubilee hailingani na kazi ya Rais mstaafu Mwai Kibaki. Kuna kasheshe inayotokea kwa sababu hakuna ajuaye kazi yake ni gani. Inakuwaje Serikali kuu inajenga barabara ya kutoka Machakos kwenda Kangundo? Gavana wa Machakos amenunua kibao kikubwa na kuweka barabarani na kusema kuwa kazi ya barabara iliyojengwa ni yake ilhali Rais anakwenda kuizindua. Kuna The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}