GET /api/v0.1/hansard/entries/722254/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 722254,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722254/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "barabara inayotoka Tala hadi barabara ya Kitui. Vile vile Gavana wa Kaunti ya Machakos ameenda na kukibandika kibao chake pale. Kazi ya barabara iwe ni kazi ya Serikali kuu. Na kama hao magavana wanataka kufanya kazi ya barabara, watolewe katika barabara kuu zote na hata ile ya ndani isisemekane kuwa barabara ya kijiji inayojengwa na gavana. Bw. Spika wa Muda, naomba kutumia neno linaloshangaza. Lami zingine zilizowekwa zinakaa kama mtu amepita akikojolea barabara na kuchukua rangi nyeusi na kuipaka juu na kuiita lami. Barabara gani ya lami isiyomaliza miezi matatu? Inastahili Serikali kuu ichukue mamlaka ya kujenga barabara. Hao magavana na wale wanaotaka kuwa gavana wajue kwamba hawastahili kamwe kujenga barabara. Pia kuna Hospitali za Level Five. Kaunti wanapewa pesa nyingi. Wenzangu hapa ni mashahidi. Huwezi kwenda Kaunti za Machakos, Kitui, Makueni, Tharaka-Nithi au Kilifi na kuonyesha pesa ya hospitali hizi imefanya kazi gani. Wanapaka rangi na kuandika kwenye kibao mlangoni: “Rehabilitated hospital” ilhali pesa iliyopeanwa na ile iliyotumika hailingani. Rais Kenyatta, isipokuwa ulisimama na kusema “wenzangu mnataka nifanye nini?” Rais, pesa inaibiwa halafu unasimama na kusema “nimefanya ninavyoweza, sasa nifanye nini?” Ikiwa kiongozi wa nchi analiuliza swali hili juu ya pesa ya Serikali – tunasikia fununu kwamba mishahara ya Wabunge, Maseneta, Mawaziri, Rais na Naibu wake inaongezwa. Ninatangaza leo kwamba tunajichimbia makaburi. Tunafikiri tunafanya vizuri na kula vizuri sana ---"
}