GET /api/v0.1/hansard/entries/722813/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 722813,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722813/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda, na kongole kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Muda. Kama wenzangu, ningependa kuchukua fursa kumpongeza Mhe. Sang. Licha ya ugumu wa nyakati tulioko za kufanya uchaguzi, yeye ameweza kuleta Mswada ambao nina imani utakapopita, utatatua matatizo yanayokumba sekta ya afya katika nchi hii. Maafisa wa kliniki wa Kenya katika nchi ya Kenya wana wajibu mkubwa sana. Mimi natoka katika sehemu kame ya Kenya; sehemu ambayo ni nadra kupata madaktari. Mengi ya matatizo ya kiafya yanayowakumba watu wetu yanashughulikiwa na maafisa wa kliniki wa Kenya. Kwa hivyo, sisi kuunda taasisi itakayowasajili, itakayoweka nidhamu, itakayowapa uwezo wa kisheria maafisa wa kliniki wa Kenya kuweza kuhudumia wagonjwa wetu, itatatua matatizo ya kiafya yanayokumba nchi ya Kenya katika sehemu nyingi. Nasikitika kwamba miaka 50 baada ya Uhuru, wafanyikazi wetu wa afya wako barabarani kufanya maandamano. Ni nyakati ambazo wangepewa kipao mbele na washughulikiwe; maanake wewe huwezi ukatibu mtu ukiwa hujui utapata chakula wapi. Uko Nairobi, gharama ya nyumba ndiyo hiyo na matatu zinaongeza bei. Huyo maafisa wa kliniki wa Kenya ama nesi atafanya vipi aende atoe huduma bila kuomba deni? Ni masuala ya haki. Ni masuala ya kuboresha mapato yao ili waweze kutoa huduma inayohitajika kwa Wakenya. Kuwaweka jela na kuwakimbiza barabarani haiwezi kuwa suluhu ya shida zinazowakumba maafisa wa kliniki wa Kenya na nesi wa Kenya."
}