GET /api/v0.1/hansard/entries/722816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 722816,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722816/?format=api",
    "text_counter": 193,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Sheria ambayo tunajadili leo inawapa uhuru na uwezo wa kisheria waweze kutatua matatizo ya matibabu yanayokumba Wakenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunazungumza juu ya mafunzo na usajili wa maafisa wa kliniki. Hapa tumepewa aina ya matatizo wanayoweza kutatua ili waweze kufungua mahospitali yao ya kibinafsi ili waweze kuhudumia Wakenya. Kiwango ambacho wamefika wako na ujuzi na wanaweza kuwahudumia Wakenya katika hicho kiwango chao. Sio lazima daktari awepo mtu anapougua malaria na homa ya kawaida, lakini ni lazima mtu atafute mtaalamu wa kutibu magonjwa hayo. Nimesimama kumuunga mkono Mhe. Sang kwa kazi nzuri aliyofanya na kuleta pendekezo hili la sheria ili maafisa wa kliniki wa Kenya waweze kutambulika na kupewa heshima na haki wanayostahili ili waweze kutekeleza kazi yao. Tukiangazia masuala ya migomo ya wafanyikazi, kuna mgomo ambao unatawala katika taifa hili. Tunaweza kuketi chini na kusikiliza malalamiko ya wafanyikazi. Hakuna mgomo ambao utawala hauwezi kuketi chini. Hii migomo inahatarisha maisha ya Wakenya. Suluhu ya matatizo yanayowakumba madaktari ingepatikana jana. Ninamuomba Rais wa Kenya aamke, aingilie kati na awaondoe madaktari kutoka barabarani awarudishe hospitalini ili waweze kuwahudumia Wakenya. Kwa hayo machache, ahsante Mhe. Spika."
}