GET /api/v0.1/hansard/entries/722833/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 722833,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722833/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru kwa kupatiwa nafasi hii ili niunge mkono huu Mswada. Naungana na Wabunge wenzangu ambao wanauunga mkono. Wakati umefika tuweze kuzungumza mambo ambayo yataweza kusaidia wale waliotuchagua. Wauguzi ndiyo wanaohudumia watu sasa katika hospitali nyingi kwa sababu hakuna madaktari. Huko kwetu mashambani, utapata wauguzi wanahudumia wagonjwa. Hao watu ni muhimu sana na wanafanya kazi nzuri sana. Kwa hivyo, naunga wengine mkono na kusema kwamba jambo hili linahitaji Bunge hili, kabla hatujaondoka, tuwe tumelitatua ili watu wetu waweze kuhudumiwa kwa njia ambayo inatakikana. Nimewasikia Wabunge wengi wakiongea. Nawaunga mkono kwamba kuna mambo nyeti na shida ambazo tunahitaji kuangalia. Nimewasikia Wabumge wengi wakisema kwamba wamejenga zahanati katika maeneo yao ya Bunge. Huko kwangu, katika sehemu ya Engashura mahali panaitwa Maili Sita, tumejenga hospitali tukitumia pesa za Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge. Pia mahali panaitwa Ndimu, tumejenga zahanati na ukienda upande za Dundori katika eneo Bunge langu, tumejenga wodi ambayo inaweza kulala watu zaidi ya mia moja. Mswada huu umekuja wakati mzuri. Jana, nilipigiwa simu na meneja wa NG-CDF eneo Bunge la Bahati akiniuliza ni wapi tutatoa pesa za kufyeka hizo zahanati kwa sababu gavana bado hajazichukua. Tukipitisha Mswada huu, tutakuwa na wauguzi ambao watawahudumia watu katika hizo zahanati. NG-CDF ilifanya kazi yake na ikamaliza. Kuna pesa tulipatiwa kupitia NG- CDF za kujenga nyumba za madaktari, ili waweze kuhudumia watu wakiwa karibu na hospitali. Sehemu nyingi kuna zahanati, lakini utaambiwa daktari au muuguzi anaishi mbali sana na yeye huja akiweza. Lakini ugonjwa unaweza kuja wakati wowote. Serikali ilikuwa na fikira nzuri na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}