GET /api/v0.1/hansard/entries/722834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 722834,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/722834/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "kwa NG-CDF, ikatupatia nafasi ya kujenga nyumba za wauuguzi ili waweze kuwahudumia wagonjwa wakiwa karibu. Mpaka sasa, kuna shida na nyumba ambazo tuliwajengea wauguzi na madaktari. Huu ndio wakati wa kuangalia ni watu wapi watakuwa wakiishi karibu na wananchi ili kuwahudumia. Wauguzi ndio wanaweza kuwahudumia watu wetu hata kwa kuwatembelea manyumbani na mitaani. Kwa hivyo, litakuwa jambo muhimu sana ikiwa Mswada huu utapitishwa haraka iwezekanavyo kwa sababu naona Wabunge wote wanakubaliana nao. Ni jambo ambalo litabadilisha nchi yetu. Watu wetu ni wagonjwa na wana shida nyingi. Juzi nilifanya medicalcamp na niliona watu wana shida nyingi sana. Kwa hivyo, lazima tuhakikishe huduma hii imepelekwa karibu na wananchi. Itawezekana tukiupitisha Mswada huu. Leo hii nilikuwa na mkutano katika Ofisi ya Masuala ya Nje. Nchi ya Qatar inataka 2,000 maafisa wa kiliniki na wauguzi kwa dharura kwa sababu wanatambua kuwa ni watu wa maana. Ile kazi wanafanya na huduma yao inasaidia sana. Lakini sisi hatuwezi kuwapa nguvu ya kufanya kazi. Kwa hivyo, naunga mkono Mbunge ambaye alileta Mswada huu. Tunahitaji kuupitisha na tuwape mamlaka ya kuweza kuhudumia watu wetu. Nashukuru sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa muda huo. Nina hakika kuwa Wabunge wote wanaunga mkono Mswada huu. Kwa sababu mengi yamesemwa, nataka niwape watu wengine nafasi kwa sababu tunazungumza kwa lugha moja. Ikiwa tunazungumza kwa lugha moja, jambo hili linahitajika sana kule mashinani."
}